
ZANZIBAR ELECTRICITY CORPORATION
(ZECO)



WITO umetolewa wa kusimamia na kutekeleza miradi kwa kasi na ufanisi ili iweze kutoa tija kwa wakati stahiki kwa maendeleo ya uchumi wa Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji Nishati na Madini Zanzibar, Ndugu: Joseph John Kilangi ameyasema hayo kabla ya kutiwa saini kwa Mkataba wa matengenezo na uimarishaji miundo mbinu ya umeme eneo la mji wa Zanzibar katika hafla iliyofanyika ofisi za Wizara Maisara, Mjini Unguja.
Katibu Kilangi amewataka watendaji wa Wizara na Idara zilizo ndani ya Wizara hiyo kuwasimamia wakandarasi wa mradi huo kutekeleza kwa wakati.
Hata hivyo, ameitaka kampuni iliyopewa kazi hiyo kuitekeleza kwa ufanisi ili waweze kupatiwa kazi nyengine za miradi ya umeme inayotarajiwa kutekelezwa na Wizara hiyo badala ya kupewa kampuni za nchi za nje.
Naye Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar, Mhandisi: Haji Haji alisema kuwa mradi huu ni miongoni mwa hatua za uimarishaji wa Mji Mkongwe wa Zanzibar ambapo utajenga vituo viwili vya kupokea na kusambazia umeme pamoja na ujenzi wa njia (33kV) za kusafirishia umeme.
Alieleza kuwa kwasasa njia za kusafirisha umeme ndani ya mji wa Zanzibar zina uwezo wa kubeba Kilovolti 11kV ambapo kupitia mradi huu njia zenye uwezo wa kilovolti 33kV zitajengwa eneo la mjini.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Miradi wa Kampuni ya Central Electricals International Limited ameihakikishia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuutekeleza mradi huo kwa ufanisi wa hali ya juuu. Aidha, ameithibitishia Wizara kuchukuwa Wazanzibari katika kutekeleza kazi za mradi huo.
Mradi huo wa uimarishaji miundo mbinu ya umeme ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa ZESTA (Mradi wa Uimarishaji Sekta ya Nishati na Upatikanaji wa Huduma ya Umeme Zanzibar) ambapo mbali na kujenga vituo vya kuzalisha na kusambaza umeme kwa kutumia nishati ya jua, kujenga njia (132kV) za kusafirisha umeme na kuwaungia wananchi umeme, kuimarisha miundo mbinu ya Mji Mkongwe ni sehemu ya utekelezaji wa mradi huu.
Sehemu hii ya utekelezaji wa mradi huu itagharimu dola za Marekani milioni 17.2 USD ambapo utahusisha ujenzi wa vituo vya umeme pamoja na kujenga mfumo wa usafirishaji umeme ndani ya Mji Mkongwe.
Msajili wa Hazina, Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya ZECO, Menejimenti ya ZECO pamoja na watendaji wa Ofisi ya Msajili wa Hazina Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza mafunzo ya Sheria ya Ofisi ya Msajili wa Hazina Zanzibar yaliyofanyika Ofisi za ZECO Gulioni tarehe 28/09/2024.
Waziri wa Mji, Nishati na Madini Mheshimiwa Shaibu Hassan Kaduara ametembelea na kukagua maendeleo ya mradi wa usambazaji umeme katika mashamba ya kilimo Kangagani kisiwani Pemba.
Kufika kwa huduma ya umeme katika mashamba hayo, yataongeza fursa za ajira kwa wakaazi wa maeneo hayo na kukuza kipato cha mtu mmoja mmjoa na Nchi kwa ujumla.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Nishati na Madini Ndg. Joseph Kilangi akiongozana na watendaji wa Wizara hiyo pamoja na watendaji wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) wakiwa katika ziara ya kutembelea mradi wa ufungaji wa vifaa vya kusawazisha umeme mdogo unaotekelezwa na Kampuni ya NOVAVIS INTERNATIONAL katika eneo la Kitogani Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.
Ufungaji wa vifaa hivyo unatarajiwa kukamilika ikifikapo mwishoni mwa mwezi wa Novemba, 2024 ingawa itaanza kufanya majaribio ifikapo mwishoni mwa mwezi wa Oktoba, 2024 na inatarajiwa kupunguza tatizo la umeme mdogo kwa asilimia 95.
Jumla ya maeneo nane (8) yanatarajiwa kufungwa kwa vifaa hivyo kama vile; Tunguu, Kitogani kwa upande wa Kusini na Mahonda, Upenja, Donge, Fukuchani kwa upande wa Kaskazini na Chuini pamoja na Ubago kwa maeneo ya Kati.
ZECO, technicians are working on the construction of an underground cable from Mkokotoni to Tumbani after the cable suffered a rupture.
The importance of this service will open investment opportunities for the island of Tumbatu.
Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) Ndg. Haji Haji akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Idara ya Huduma za ufundi na uzalishaji umeme Mhandisi Moh'd Zuber juu ya namna ufanyaji kazi wa kituo cha kupozea na kusambazia umeme kiliopo Mpendae Zanzibar.
Ziara hiyo imempa uwelewa Meneja Mkuu kujua changamoto mbali mbali zinazoikabili miundo mbinu ya umeme hapa Zanzibar.
Mafundi wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) wakiwa katika kazi ya usambazaji umeme katika mashamba ya kilimo katika kijiji cha Umbuji kinachopatikana Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Kazi hiyo ya usambazaji umeme itawanufaisha wakulima hao kwa kuweza kufanya kazi zao za kilimo cha umwagiliaji maji kwa siku zote za mwaka.
Aidha, huduma ya umeme itaweza kufungua fursa za ajira kwa wakaazi wa maeneo hayo.
Waziri wa Wizara ya Maji, Nishati na Madini Mheshimiwa Shaib Hassani Kaduara, Mkurugenzi Idara ya Nishati na Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar pamoja na watendaji wa Wizara wamefanya ziara ya kukagua njia kuu ya kusafirishia umeme wa msongo wa 132 kilovolti ambapo watu wasiojulika wameiba vyuma vya miundo mbinu hiyo.
Waziri wa Wizara ya Maji, Nishati na Madini Mheshimiwa Shaib Hassan Kaduara (ambae hayupo pichani) akizungumza na wafanyakazi wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) wakati wa mkutano wa kila mwaka wa kuzungumza na wafanyakazi hao.
Naibu Waziri wa Wizara ya Maji, Nishati na Madini Mheshimiwa Shaaban Ali Othman amezindua huduma ya umeme kwa wakulima wa Dongwe Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.