UKAGUZI WA MIUNDO MBINU ILIYOIBIWA VYUMA
Waziri wa Wizara ya Maji, Nishati na Madini Mheshimiwa Shaib Hassani Kaduara, Mkurugenzi Idara ya Nishati na Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar pamoja na watendaji wa Wizara wamefanya ziara ya kukagua njia kuu ya kusafirishia umeme wa msongo wa 132 kilovolti ambapo watu wasiojulika wameiba vyuma vya miundo mbinu hiyo.