Shirika la Mafuta na Nguvu za Umeme (SFPC) lilianzishwa mwaka wa 1964 chini ya iliyokuwa Wizara ya Maji, Ujenzi, Ardhi na Mazingira kwa Sheria nambari 12 ya mwaka 1964. Shirika lilianzishwa kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya umeme na utoaji wa huduma ya umeme katika visiwa vya Zanzibar. Sekta ya umeme ilifanyiwa mabadiliko kwa mara nyengine tena mabadiliko ambayo yameiondosha Shirika la Mafuta na Nguvu za Umeme mnamo mwaka wa 2006 na kuanzishwa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) katika kusimamia shughuli zote zinazohusiana na nishati ya umeme Zanzibar kwenye kuzalisha, kusambaza na kugawa umeme katika visiwa vya Zanzibar.

Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) linamilikiwa kwa asilimia 100 na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Ardhi,