Shirika la Umeme Zanzibar katika hatua ya kuimarisha utendaji kazi wa miundombinu yake ya kusambaza umeme inatarajia kufanya matengenezo  ya Transfoma zake mbili kubwa ziliopo katika kituo cha Umeme Mtoni Zanzibar.

Matengenezo hayo yanatarajiwa kufanywa kwa siku ya Jumamosi tarehe 20/04/2019 na Jumapili tarehe 21/04/2019, hivyo kutakuwepo na uzimaji wa umeme wakati wa matengezo transfoma moja kwa kila siku moja hivyo kutokana na mahitaji halisi ya utumiaji umeme kutakuwepo na upungufu wa umeme kwa baadhi ya maeneo katika siku mbili hizo.

Ili kuwawezesha watumiaji wa umeme kuendelea na shughuli zao za uzalishaji mali na za kijamii,Uongozi wa ZECO utalazimika kugawa umeme kwa mgao kwa siku mbili hizo kwa utaratibu maalumu.

Kupata ratiba kamili ya mgao huo tafadhali bonyeza hapa

IMETOLEWA

KITENGO CHA UHUSIANO

SHIRIKA LA UMEME ZANZIBAR

ZECO

18/04/2019