Shirika la umeme Zanzibar (ZECO) limeahidi kuendelea kuwa karibu na jamii yenye uhitaji wa masuala mbali mbali ikiwemo sekta ya afya ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika sekta hiyo.
    ZECO ikiwa ni taasisi inayotoa huduma imeona umuhimu wa kusaidia sekta ya afya kwa kukabidhi vifaa vitakavyosaidia kuweka usafi katika kituo cha afya chumbuni ambapo afisa uhusiano wa shirika la umeme Zanzibar Salum Abdalla Hassan amesema kufanya hivyo ni kutimiza wajibu wake kwa jamii.
Akipokea msaada huo Mkurugenzi msaidizi wa Baraza la manispaa Dk. Ramadhan Mikidadi amesema baraza linafarijika kuona wadau mbalimbali wanajitokeza kusaidia masuala ya usafi.
Daktari dhamana wa kituo cha afya Chumbuni Dk. Mohamed Muslim Muhamed amesema ni wakati muafaka kupata msaada huo ikizingatiwa kuwa hali ya mvua imeanza na itasaidia kuweka mazingira safi, huku sheha wa sehia ya Karakana Bakari Makame Omar akisisitiza umuhimu wa wananchi kuthamini usafi.
                                                                                                              
                                                                   
Afisa Uhusiano Shirika la Umeme Zanzibar  (ZECO) Salum A. Hassan (wanne kulia) akimkabidhi vifaa vya usafi Mkurugenzi Msaidizi Baraza la Manispaa Zanzibar Ramadhan Mikidadi kwa ajili ya
                                                                                          matumizi katika kituo cha afya Chumbuni.
 
                                                                    
  
Daktari dhamana kituo cha afya Chumbuni Muhamed Muslim Muhamed akifurahia jambo wakati wa makabidhiano ya vifaa vya uasafi vilivyotolewa na shirika la umeme Zanzibar kwa kituo hicho  cha   afya, wengine wanaoshuhudia ni Mkurugenzi Msaidizi baraza la manispaa na wafanyakazi wa kituo cha afya Chumbuni.